• Breaking News

  Aug 12, 2016

  Mashabiki wa Mziki Wamjia Juu Harmonize Wamtaka Aache Kumwiga Diamond...


  Mashabiki wa muziki wa bongo fleva wamemjia juu msanii Harmonize wakimtuhumu kumuiga Diamond Platnumz, kwenye kazi zake hadi mavazi.


  Malalamiko hayo yamezidi kushamiri baada ya msanii Dully Sykes kuachia video ya Inde aliyomshirikisha Harmonize, ndipo mashabiki kuamua kutoa yao ya moyoni, baada ya kuona jinsi alivyokuwa akicheza mpaka uimbaji wake, na kumtaka awe mbunifu kwa mitindo yake mwenyewe.

  "Harmonize try to do your Own Style at LIST Don't copy everything from Diamond even ya in Same WSF at Least Do your Style to Inspire your fans, but still love you",... aliandika shabiki aliyejulikana kwa jina la Nadia Nadia.

  "Harmonize anakopi kila kitu kwa Diamond. Inachosha".....aliandika shabiki mwengine Kennedy Daima Mmari.

  Naye Ruth Murira aliandika....."Hermonize pliz try to do it ur own way, styles ni za Mondi, kavalia pia ka Diamond, for a moment i thought its Diamond,aaaaish".

  Tatizo hili si mara ya kwanza kujitokeza kwa msanii huyo, huku wengi wakisema kuwa chini ya Diamond haina maana aige kila kitu kutoka kwake, hata kama ndiye mtu anayemuangalia kisanaa (role model), kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anaficha kile alichonache yeye kama Harmonize, na kuuvaa u-Diamond.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku