Aug 7, 2016

Matamko ya Prof. Ndalichako Yanatuchanganya

Ndalicho
Wengi mmeona habari ya leo kuwa sasa ni lazima wanafunzi wote wasome Sayansi kabla ya hiii zimekuwepo habari nyingi za kushangaza za wizara hii ya elimu. Siku Magufuli aliposema anashangaa fimbo kupigwa marufuku mashuleni, kesho yake tu Wizara hii ikatangaza 'fimbo kurudishwa mashuleni'

yaani halikuwa na mjadala wala kutolewa maelezo labda why fimbo zilizuiwa mwanzo au kuna watalaam gani walihusika kufikia maamuzi.

Halafu yakaja maamuzi ya kuongeza ufaulu ili kujiunga na vyuo, hili nalo limechukuliwa kama Tanzania ni kisiwa vile mpaka sasa wala hakuna maelezo iwapo mwanafunzi wa kitanzania akipata nafasi kusoma nje ya nchi kwa ufaulu ambao hapa nchini haumruhusu, vyeti vyake vitakuwa na 'status' gani hapa nchini mradi maamuzi ya wizara hii sasa ni kama vile Tanzania ndo 'The world'
na kila atakachoamua yeye ndo 'final'

Huyu mama na Mabosi zake wanasahau kuwa tuko katika 'global village' Maamuzi ya ajabu ajabu sanasana yatawaathiri watoto wa masikini tu
wengine wenye options za kusoma nchi jirani na nchi za mbali hayatawagusa na mwishowe watakao 'umizwa na maamuzi' haya ni watoto wa masikini.Sasa hili la lu kulazimisha Sayansi nalo unajiuliza nchi ngapi duniani linatumika?

Je mtoto wa kitanzania akisoma Kenya au Uganda au kwingineko
ambako hakuna 'maamuzi ya aina hii' huyu mama atafanyaje? Hivi why 'tuna invest kwenye kuongeza kero na vizingiti' vya kila aina kwa watanzania? Kwani Tanzania ni kisiwa? Si masuala ya elimu yanapaswa kuwa 'Universally acceptable'? Sasa huyu mama ndo mifano wa maprofessa wetu?

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR