• Breaking News

  Aug 3, 2016

  Mbaroni Akidaiwa Kufyatua Risasi Ovyo...

  Mfanyakazi mmoja wa Kampuni ya Marenga Investment ya mjini Moshi amekamatwa na polisi kwa kosa la kufyatua risasi ovyo baada ya gari lililokuwa mbele yake kutomruhusu kupita kwa wakati.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema jana ameagiza mfanyabiashara huyo anyang’anywe silaha na kufunguliwa mashtaka ya matumizi mabaya.

  Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki eneo la Rongai wilayani Rombo na ofisa huyo alilifyatulia gari hilo risasi mbili ambazo hazikuleta madhara.

  Amedai kuwa siku hiyo saa 11:30 jioni, mtuhumiwa huyo akiwa na watu wengine watatu katika gari aina ya Suzuki Escudo, alilifyatulia risasi gari aina ya Mitsubish Canter.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku