• Breaking News

  Aug 1, 2016

  Mbowe na CHADEMA, lini mtatuomba radhi watanzania kuwa mlidanganya Lowassa sio fisadi

  Ndani ya miaka nane na zaidi wananchi tumeimbishwa na kuaminishwa usiku na mchana kuwa Lowasa ni Fisadi mkubwa wa uchumi wa Tanzania.

  Na mbaya zaidi mkasema mnaushaidi wa ufisadi wa Lowassa kama anabisha aende mahakamani.

  Wengi tuliamini na mpaka sasa tumesimama kwenye misingi ya uaminifu kuhusu Chadema kuwa Lowasa ni Fisadi na hafai kupewa nchi.

  Lakini wengi wetu mmeshindwa kutushawishi kwa hoja kwa nini Lowassa awe msafi sasa.

  Ni vema mtuombe radhi hadharani kuwa ndani hiyo miaka mlikuwa mnatudanganya na kutulaghai ili kuwalaghai na ccm wamteme Lowassa.

  Bado nipo kwenye misingi ya awali ya Chadema kupinga ufisadi na mafisadi na naamini Lowassa ni fisadi mpaka pale viongozi wa Chadema mtakapokiri wazi kuwa mlitupotosha Lowassa sio fisadi na ushahidi mlikuwa hamna.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku