Aug 10, 2016

Mbunge Ester Bulaya Amwaga Mamilioni ya Fedha Bunda

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya ametoa Sh15 milioni kwa ajili ya kuviimarisha kiuchumi vikundi 15 vya akiba na mikopo jimboni humo.

Pia, Mbunge huyo ametoa msaada wa pikipiki mbili zenye thamani ya Sh4 milioni kwa Kikundi cha Vijana cha Ulipo Tupo cha mjini Bunda kama moja ya vitega uchumi. Kikundi hicho kinajishughulisha na masuala ya ujasiriamali na uwezeshaji vijana.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi fedha na pikipiki hizo juzi, Bulaya alisema lengo ni kuwajengea wananchi uwezo kiuchumi kupitia mikopo midogomidogo na ujasiriamali.

“Huu ni utekelezaji wa ahadi zangu za kampeni ya kuanzisha na kusaidia vikundi vya maendeleo Bunda,” alisema.Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com