• Breaking News

  Aug 29, 2016

  MBUNGE Godbless Lema Aeleza Kwanini Amekataa Kula Chakula Rumande

  Godbless Lema Hospitalini
  Tangu alipokamatwa Agosti 26, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alikataa kula chakula baada ya ombi la dhamana yake kukataliwa hivyo akalazimika kulala rumande.

  Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA mkoa wa Arusha, Kalist Lazaro alipokutana na waandishi wa habari leo amesema kuwa wanaliomba Jeshi la Polisi limuachie mbunge huyo kwani hali yake ni mbaya ukizingatia hajala chochote tangu aliposwekwa rumande.

  Naliomba Jeshi la Polisi limuachie kwa sababu akifa au kupata madhaa mengine wakiwa humo ndani, linaweza kukuza ukubwa wa tatizo na ukizingatia kuna maandamano tuliyopanga Septemba 1, hivyo akipata tatizo lolote watu wanaweza kufanya vurugu, alisema Kalist Lazaro.

  Kuhusu suala la dhamana, Jeshi la Polisi limesema kuwa haliwezi kumpa dhamana kwa sababu upelelezi bado unaendelea.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu huyo, Mbunge Godbless Lema amekataa kula kwa sababu anaona kuwa anaonewa kunyimwa dhamana ambayo ni haki yake, lakini pia ameeleza kuwa alidhalilishwa wakati alipokamatwa.

  Amesema kuwa yupo tayari kula, endapo atapelekwa mahakamani.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku