Aug 4, 2016

Mbwana Samatta Aikaribia Ueropa League...Kupambana Usiku wa leo


Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo atakuwa anawania tiketi ya kwenda hatua ya makundi ya Europa League wakati timu yake, KRC Genk itakapomenyana na wenyeji Cork City FC katika mchezo wa marudiano Raundi ya Tatu ya mchujo.

Genk inahitaji kulazimisha sare kwenye Uwanja wa Turner's Cross, mjini Cork, Ireland baada ya awali kushinda 1-0 Alhamisi iliyopita nyumbani.

Pamoja na ugumu uliopo mbele yao, Samatta amesema wanakwenda kutafuta mabao na kujilinda zaidi.
"Tutapambana, maana kwenye mchezo wa marudiano tunatakiwa kwenda kutafuta mabao na kujilinda, tutajitahidi"

Timu zitakazoshinda zitakwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi, ambako vigogo kama Manchester United ya England wataanzia huko.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR