• Breaking News

  Aug 6, 2016

  Mgeja Ampinga Rais Magufuli

  ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema hatua ya Rais John Magufuli kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini, imelenga kuminya demokrasia na serikali kutaka kutokosolewa.

  Mgeja, ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo haikubaliki katika nchi ya kidemokrasia duniani kwa kuwa uhai wa vyama vya siasa upo katika mikutano.

  Pia amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kushughulikia migogoro ya vyama badala ya kusubiri hadi nchi ikielekea katika mgogoro mkubwa.

  Alisema kauli ya Rais Magufuli kwamba shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020, inakiuka katiba kwa kuwa mikutano na shughuli za vyama vya siasa vipo kikatiba.

  Alieleza kuwa kinachotokea sasa kwa viongozi wa upinzani ni kupigania demokrasia hali ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

  “Serikali inakosolewa kupitia mikutano ya vyama vya siasa na serikali isitupangie cha kuzungumza. Kutokana na kauli ya rais tunaonya likitokea lolote katika mikutano ambayo itafanyika nchi nzima, kupitia operesheni ya Umoja wa Kuondoa Udikteta Tanzania (Ukuta), Rais atawajibika iwapo nguvu ya jeshi polisi itatumika,” alisema.

  1 comment:

  1. Huu si uchochezi. Huyu ni mtu mwenye busara na anatoa ukweli uliopo. Kuna madhara makubwa kwa raisi kutumikia chama chake badala ya serikali ambayo ni watu wa vyama vyote waliomweka madarakani. Mtu mmoja hawezi kuzima uhuru wa mamilioni ya Watanzania. Ni mtu mmoja zidi ya mamillioni ya watu. Hii inaleta mgawanyiko , mpasuko na itakuwa chanzo cha tatizo kubwa nchini lisiloingika. Mamilioni ya watu wenye elimu, busara, utashi hawawezi kuwekwa mabubu na mtu mmoja. Ni shujaa tu ataona ukweli wa hii. Raisi hakuchaguliwa kukatazaviongozi wengine wasizungumze. Raisi hawezi kuiongoza nchi peke yake. Ye si Mungu, hata Mungu aliwatuma mitume duniani kote kwa niaba kueneza neno lake. Iwe binadamu.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku