• Breaking News

  Aug 8, 2016

  MH.Rais Magufuli Anabadili Gia Angani?

  Rais Magufuli ameonekana kua tofauti na kauli zake ambazo aliku akizitumia katika kampeni zake.

  Nikianza na kauli yake aliyokua akipinga suala la ushuru kwa kusisitiza "sitaki kusikia ushuru, ushuru katika watu wadogo wadogo wadogo"alizungumza maneno haya katika mkutano mkuu wa kampeni mkoa wa mwanza uliofanyika uwanja wa CCM-kirumba.
  Nanukuu"Uwe unauza tu nyanya ushuru,uuze tu miwa ushuru,unakwenda kunyoa ushuru,unaenda saluni ushuru,ata kama unabrashi viatu ushuru,unaziba tairi ushuru,una boda boda ushuru.Haya maushuru ×4 tunataka tuyafunge ili serikali ya awamu ya tano isitegemee ushuru kwa watu wadogo ×2" mwisho wa kunukuu.

  Katika kauli hiyo apo juu Mh Rais nazani alishawishi idadi kubwa ya wananchi wa hali ya chini kumchagua kutokana kupinga "ushuru kwa watu hali ya chini" lakini kwa sasa hali ilivyo ni tofaut Mh.Rais kabadili gia angani.

  Nikianza na swala boda boda kwa sasa wanahangaika tu na kulalamika kutoka na kuongeza kwa ushuru,akina mama wenye biashara ndogo ndogo kama vile wauza mazao,nyanya,samaki,mamantilie N.k wanahangaika tu kutwa kucha wanafukuzana na maaskari au mgambo pia bei hairidhishi sokoni ila kwakua maisha magumu hawana namna inabidi wauze tu.Sasaivi ukienda sokoni ukiingiza mzigo ndani ya soko wanadai ushuru ,sehem unapoweka mzigo ili uuze utadaiwa pia, halii inawafanya watu wa hali ya chini wahangaike na kushindwa kuuza biashara zao au kuambulia hasara na kufanya maisha yao kua magumu.

  Kwa sasa wananchi waliopo vijijini hawana namna zaidi ya maisha magumu wanayoyapata na hivo kukaa wakiulizia "hivi million hamsini za kila kijiji zinakuja lini?"madiwani ,wabunge wenyekiti wa vijiji na mitaa hawana majibu.
  Kwa hali ilivyo sasa vijijini million hamsini za kila kijiji zipelekwa ili kuweza kuwanusuru watu wa hali ya chini.
  Huu ni utafiti mdogo tu nilio ufanya katika mikoa ya kanda ya ziwa.
  (Kigoma,mwanza ,kagera ,shinyanga ,Simuyu na baadhi ya viji vya Tabora).

  Jamii Forums

  1 comment:

  1. Wananchi vijijini hawana usawa. Wanatumika mara nyingi sana kudanganywa ili wachague ccm. Zamani walikuwa wamipata vitenge au kanga. Kutumia umaskini wa mtu kwa kuchaguliwa ni dhambi kwa Mungu. Marsisi wamekuwa wa mijini na matajiri na wakanja wachache.wamiingia madarakani wsmeshashiba na mujisahau. Kwani wapo karibu na matajiri kila siku. Liambiwa, mtu mmoja hawezi kuleta maendeo ya kweli bila kubadili mfumo wa chama ambacho kinawstumikia mataniri kwa sasa. Wsmesahau na maisha safi wanayoyaishi kila siku.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku