• Breaking News

  Aug 19, 2016

  MICHEZO KRC Genk Imelazimishwa Sare na Lokomotiva Ugenini, Samatta Apachika Bao

  Usiku wa August 18 2016 michezo ya Play offs ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Europa League ilichezwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, moja kati ya michezo ya Europa iliyochezwa usiku wa August 18 ni mchezo kati ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia dhidi ya KRC Genk inayochezewa na Mbwana Samatta.

  Katika mchezo huo uliyochezwa Croatia yaani katika uwanja wa nyumbani wa Lokomotiva, umemalizika kwa sare ya goli 2-2, Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilianza kupata goli la kwanza kwa mkwaju wa penati kupitia mjamaica Leon Bailey dakika ya 47 na baadae Mbwana Samatta dakika ya 52.

  Licha ya kuwa Lokomotiva walikuwa nyumbani na kufanikiwa kusawazisha goli zote mbili kupitia kwa Mirko Maric dakika ya 51 na Ivan Fiolic dakika ya 59, KRC Genk ilitawala mpira kwa asilimia 60 na kuwaacha wenyeji wao wakimiliki mpira kwa asilimia 40, Kwa matokeo hayo Genk itahitaji suluhu au sare ya goli 1-1 katika mchezo wa marudiano August 25 katika uwanja wao nyumbani.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku