Aug 16, 2016

Mke Auawa Kwa Kupigwa Nyundo Kichwani na Mumewe Baada ya Mchepuko Kupiga Simu Usiku

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Monica Manyabhuluba mkazi wa kijiji cha Busungo kata ya Segese wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa nyundo kichwani na mme wake Deus Shitungulu

Diwani wa Kata ya Segese, Joseph Manyala amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo.

“Chanzo ni wivu wa mapenzi kwani mwanamme alipigiwa simu usiku na mwanamke mwingine, mkewe (Monica) akamuuliza mmewe huyo mwanamke anayekupigia simu usiku huu ni nani ndipo ugomvi ukaibuka na hatimaye jamaa akamuua mke wake kwa kumpiga nyundo kadhaa kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo”, amesema diwani huyo.

“Kichwa cha mwanamke huyo kimebondeka kwa kupigwa nyundo, kwa kweli tukio hili linasikitisha sana, polisi wamefika eneo la tukio mchana huu”, amesema Manyala.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR