Aug 22, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman Astaafu, Nafasi Yake Yakaimiwa na George Madafa

KURUGENZI Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Rashid Othman amestaafu rasmi wadhifa huo.

Amestaafu rasmi wadhifa huo Agosti 19, mwaka huu akiwa ameiongoza taasisi hiyo tangu Agosti 20, 2006 ikiwa ni takribani miaka 10.

Kiongozi huyo aliteuliwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu ili kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa wakati huo, Cornel Apson Mwang’onda.

Aliapishwa Ikulu Dar es Salaam Agosti 21, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Othman alikuwa Mkuu wa Utawala na Utumishi wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa na kufanya kazi nzuri, iliyochangia kumwezesha kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.

Awali, Othman alitakiwa kustaafu mwaka 2013 kwa mujibu wa sheria, lakini aliendelea kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja hadi alipokubaliwa kustaafu rasmi Ijumaa iliyopita. Othman atakumbukwa kwa kazi nzuri, aliyoifanya kwa Taifa tangu alipoingia katika utumishi wa umma.

Chanzo cha kuaminika kimeliambia Gazeti la Mtanzania kuwa nafasi ya Rashid Othman kwa sasa inakaimiwa Mkurugenzi wa Mambo ya Ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa, George Madafa.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR