Aug 1, 2016

Moto uliozuka Sinza jana wasababisha hasara ya dola milion moja na elfu ishirini

Moto mkubwa uliozuka jana katika kampuni ya Usafirishaji ya Highyway ya Sinza jijini Dsm umesababisha hasara kubwa ya karibu dola milion moja na elfu ishirini kutokana na kuungua kwa Vipuri vya magari,injini za magari,matairi mapya ya magari makubwa zaidi ya 300 pamoja na mapipa ya mafuta ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika.

Akizungumza na Chanel ten majira ya Asubuhi Afisa Mwajiri ya kampuni hiyo ya Usafirishaji Solomon Mahogo amesema moto huo ambao umeteketeza mali nyingi ulifanikiwa kudhibitiwa saa nane Usiku kutokana na Changamoto ya Kuishiwa maji magari ya halmashauri ya jiji yaliokuwa katika kazi ya Kuzima moto huo.

Aidha amesema pamoja na Kuwapo vifaa vingi vya kuzimia moto katika eneo hilo ambalo pia kuna Visima vya mafuta bado kuna hitajika kazi ya ziada katika kupambana na majanga ya moto ikiwemo kuwapo vifaa vya kisasa vya kudhibiti moto

Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com