• Breaking News

  Aug 2, 2016

  Msaga Sumu: Man Fongo acha kuniiga


  Muanzilishi na mfalme wa nyimbo za singeli Msaga Sumu kama mwenyewe anavyojiita amesema yeye hajali bifu ambazo wasanii wenzake wa visingeli wanazomuundia


  Akizungumza ndani ya eNewz amesema “ huwezi ukaamini bifu na mimi wameanza tangu naanza ni kweli wanakuja na wapo wengi hao watoto lakini naweza kuwaambia bifu na mimi wanashindwa kwa sababu mimi ni mtu ambaye naangalia maisha kuliko bifu.


  Mimi ninachokumbuka nilimuambia kama anataka muziki uwe wa maisha yako jifunze kukomaana mi naona ameamua kuzingatia kwa kuwa naona wimbo wake huu wa 'hainaga ushemeji' kidogo umepita japo haujazidi wimbo wangu wa “Shemeji unanitega” aliendelea kusisitiza Msaga Sumu.


  Msaga sumu alimalizia kwa kusema “naweza kusema ndo maana wananiwekaa juu kwa maana kila ninapotoa mimi na wao wa wanafata hicho hicho yaani hawana ubunifu ninachotaka kuwaambia kama wanataka kuja ili mziki wa kisingeli ufike mbali wajitahidi kubuni na si kusubiri Msaga Sumu abuni alafu waige.


  Hata hivyo kwa upande wa Man Fongo aliisema “Mimi naangalia alama za nyakati naangalia mziki unaelekea wapi na mimi sitaki ufalme wala nini na kama wapo walioanza sitaangalia walianzia na ladha mimi naimba singeli hivyo sitaangalia anachokifanya mtu yeyote.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku