• Breaking News

  Aug 23, 2016

  Msajili wa Vyama Awaasa Wanaopanga Kuandamana

  Vyama vikuu vya siasa vimeleta sintofahamu na kuzua hofu kwa wananchi baada kutangaza kufanya maandamano, kwa mujibu wa msajili wa vyama nchini, Jaji Fransis Mutungi.

  Jaji Mutungi ameyasema hayo Jumanne hii jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema migogoro na changamoto za kisiasa zinazovikabili vyama vya siasa visipojadiliwa vizuri katika meza moja ya majadiliano baina ya pande mbili, inaweza kusababisha kuvunjika kwa amani ambayo imejengwa kwa muda mrefu na waasisi wa taifa.


  “Vyama vya siasa nchini vyenye mpango wa kufanya maandamano au mikutano ya kuhamasisha wanachama wake, viache ili kutafuta suluhu za changamoto zinazowakabili kupitia majadiliano hayo ya pamoja,” alisema Mutungi.

  Alivitaka vyama vya siasa kutumia mkutano maalumu wa baraza la vyama vya siasa unaotarajiwa kufanyika Agosti 29 na 30 mwaka huu kujadili changamoto zinazowakabili kwa njia ya amani na maridhiano badala ya kufanya maandamano ambayo yanaweza kuhatarisha amani ya nchi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku