Aug 29, 2016

MSEMAJI wa CCM Ole Sendeka Amsifu Lowassa Baada ya Kusalimiana na Magufuli

Lowassa na Magufuli
Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka amesema Edward Lowassa ni muungwana na kwamba asingeweza kuacha kumsalimia kwa kumpa mkono Rais John Magufuli.

Ole Sendeka amesema jana: “Namfahamu Lowassa ni muungwana hawezi kuacha kusalimiana kwa kupeana mkono na Rais. Wamekutana viongozi, Rais na waziri mkuu mstaafu hawawezi kuacha kusalimiana.”

Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema aliyechuana na Rais Magufuli katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 mwaka jana, juzi walikutana kwa mara ya kwanza na mpinzani wake huyo tangu kinyang’anyiro hicho kilipomalizika.

Viongozi hao walikutana kwenye misa ya jubilei ya dhahabu ya ndoa ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na mkewe Anna katika Kanisa la Mtakatifu Petro.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR