• Breaking News

  Aug 3, 2016

  Mtuhumiwa wa Kumuweka Rehani Nduguye Nchini Pakstan Apandishwa Kizimbani

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam imempandisha kizimbani Mtuhumiwa Juma Abdallah Mwinyi aliyehusika kumuweka rehani ndugu yake nchini Pakistani ,na kusomewa shitaka la kufanya Biashara Haramu ya kusafirisha Binadamu.

  Akisomewa shtaka hilo na wakili wa Serikali Peter Njika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha amesema kuwa mtuhumiwa Juma Abdallah Mwinyi kati ya Mwezi januari mwaka 2015 na Julai mwaka 2016 katika jijin la Dar es Salaam alifanya kosa hilo kwa madai ya kutoa mafunzo alimsafirisha ndugu yake kwenda nchini Pakistani.
  Mtuhumiwa huyo,amekana shitaka hilo Wakili wa serikali Njika amesema upelelezi bado unaendelea
  Hakimu Mfadhidhi Mkeha amesema Shauri hilo halina dhamana,Mtuhumiwa amerejeshwa Rumande mpaka Agost 17,kesi hiyo itakapotajwa tena.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku