• Breaking News

  Aug 26, 2016

  Mufti Mkuu: Masheikh wa Mitandaoni ndio Wanaopinga Makonda Kutujengea BAKWATA Ofisi

  Mufti Mkuu
  Akiongea ktk sherehe za uzinduzi wa Jiwe la Msingi la jengo la BAKWATA,Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Zubeir anasema wale Masheikh wote wanaopinga Mkuu wa mkoa wa Dsm kuwajengea jengo BAKWATA ni "Masheikh wa Instagram na WhatsApp" ambao wana husuda juu ya maendeleo ya BAKWATA na hivyo kupinga hatua hiyo yenye heri kutoka kwa mkuu wa Mkoa.

  Mufti Zubeir anasema kumezuka wimbi la "Masheikh na Waislam wa Instagram" ambao wanasema ni kosa kwa msaada wa jengo la BAKWATA kutoka kwa mkuu wa mkoa ambaye si wa dini yao.Mufti Sheikh Zubeir ametoa mifano tofauti ya misikiti ambayo waislamu wengi wanaitumia na wakati ilijengwa kwa msaada na hamasa ya watu wasio wa dini yao.

  Mufti Zubeir anasema msikiti wa Ghadafi uliopo Dodoma ulijengwa na Rais Ghadafi kwa hamasa na chagizo la Rais Benjamin Mkapa.Pia msikiti uliopo Butiama ulijengwa na kuhimizwa na mwalimu Nyerere kwa ajili ya waumini wa kiisalam waliopo kijijini kwake,hii haiondoi ukweli kuwa aliyejenga si wa dini hiyo lakini bado ni halali kuwa nyumba ya ibada.

  Msikiti wa Kwa Mtoro ni zao la Governor wa Kikoloni ambaye alikuwa mzungu na mkristo,misikiti katika mashamba ya mkonge maeneo ya Korogwe,Muheza na maeneo ya Same ilijengwa na wakoloni kwa ajili ya "manamba" kuweza kupata sehemu ya ibada,na kwa kujengwa kwake na Wakristo au watu wasio waislamu haiondoi uhalali wa kuwa nyumba ya ibada.

  Mufti anasisitiza kuwa kama hao "Waislam wa Fb na instagram" wanaona vibaya kwa BAKWATA kujengewa msikiti,basi waache na kupewa huduma nyingine za kijamii zinazotolewa na watu wasiokuwa wa dini yao,anasema mtu unaenda ardhi kuchukuwa hati ya nyumba au ardhi na imewekwa saini ya "JOHN" hasemi sitaki kwa sbb ya hii saini,ila akiona BAKWATA inapewa msaada na RC wanasema "haifai kwa sababu msikiti hauwezi jengwa na mtu asiye wa dini hiyo".

  Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwaagiza watumishi wa umma kuwaheshimu viongozi wa kidini na kuwapa kipaumbele wanapokuwa wanasaka huduma ktk ofisi za kijamii.Mh.Makonda anasema tayari amepatikana mkandarasi wa kujenga jengo la BAKWATA ambalo litaleta heshima kwa Tz na waislamu wa Tanzania.

  Amewaonya "masheikh,wachungaji na maaskofu wa istagram" waache mara moja kuwa na husda kwa yeye kutoa msaada wa jengo kwa BAKWATA.Jengo hilo litakuwa na ghorofa tatu yenye maktaba ya vitabu na kompyuta.Ofisi ya Mufti,Sheikh wa mkoa wa Dsm na baraza la Waislamu la kina mama.

  Makonda anasema wanaoongoza kwa kumpa misaada ya kimaendeleo kwa mkoa wa Dsm ni waumini wa dini ya kiislamu,akitolea mfano wa mtu mmoja kujitolea kujenga ward tatu zenye ghorofa katika hospitali za Temeke,Ilala na Kinondoni.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku