• Breaking News

  Aug 19, 2016

  Muhongo Atoa Agizo Zito Tanesco

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ametoa agizo kwa ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutoa elimu kila nyumba ili ifikapo mwaka 2020 makazi yote yawe yanatumia nishati hiyo.

  Ametoa agizo hilo alipotembelea miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) na kukutana na wananchi waliolalamika kuwa hawana elimu ya kutosha kuhusu umeme.

  Profesa Muhongo amesema Serikali imejiwekea malengo kuwa ifikapo mwaka 2020 kila Mtanzania awe anatumia umeme na Serikali kuuza nje ya nchi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku