• Breaking News

  Aug 16, 2016

  Muumini Auawa Baada ya Mchungaji Kushindwa Kufanya Miujiza...


  Katika harakati za kuonyesha miujiza ya Mwenyezi Mungu, Mchungaji mmoja kutoka huko Afrika Kusini, katika Kanisa la ‘The Mount Zion General Assembly’ aliyejulikana kwa jina la Lethebo Rabalango, kushindwa kuonyesha miujiza hiyo iliyoishia kwa mwanamke ambaye ni muumini wa kanisa lake kupoteza maisha baada ya kuwekewa spika nzito juu ya mwili wake alipokua amelala chini.

  Mchungaji Lethebo Rabalango alimwalika mwanamke mmoja kwenye jukwaa na kumwambia alale chini na kisha kuaamuru wasadizi wake kumuwekea spika ya redio kubwa yenye uzito wa kilo 113.4,  na kama hiyo haikutosha Mchungaji huyo akapanda na kukaa juu huku akisema mwanamke huyo hatapata maumivu yoyote kwa ajili ya nguvu na uwezo aliyonao Mungu. Na cha kushangaza mwanamke huyo alipoteza maisha papo hapo kutokana na uzito wa spika ile kusababisha madhara kwenye mfumo wa upumuaji wake

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku