• Breaking News

  Aug 7, 2016

  Mwakyembe: Tuna nia nzuri kuikatia rufaa hukumu ya umri wa wasichana kuolewa

  Baada ya serikali kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kipengele cha umri wa mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 kwamba kinakiuka katiba kwa nia ya kuufanya uamuzi huo kuwa sheria.


  Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe aliyasema hayo Ijumaa hii jijini Dar es Salaam alipokutana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) ambao walimtembelea ofisini kwake kuzungumzia mambo kadhaa likiwemo suala hilo la serikali kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

  Pia uamuzi wa Mahakama Kuu uliitaka serikali kufuta vifungu viwili cha 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 vinavyoeleza mtoto wa miaka 14 na 15 anaweza kuolewa kwa idhini ya mzazi au Mahakama.

  Dk Mwakyembe alisema, “Serikali imeamua kukata rufaa Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi huo si kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, bali kupata uamuzi wa chombo cha juu cha Mahakama ambao hautaweza kubadilishwa na hivyo kuwa kama sheria”,alisema.

  “Serikali inapingana na uamuzi wa Mahakama Kuu ila kinachofanyika ni utaratibu wa kawaida ambao utaiwezesha Serikali kuwa na uamuzi kutoka katika chombo cha juu kabisa cha Mahakama nchini,”, aliongeza.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku