• Breaking News

  Aug 15, 2016

  Mwanamume Apewa Kichapo Kwa Kufanya Mapenzi na Dadake

  Mwanamume mmoja mkazi wa Kibera Kenya alipewa kichapo cha mbwa baada ya kuambiwa kuwa mke aliyekuwa amempeleka nyumbani kwao ni binamu wake.

  Jamaa mmoja kutoka Nyanza amepewa kichapo na babake mzazi na baadhi ya wazee wa jamii yake kwa kujaribu kuitetea ndoa yake ya miaka miwili ( na binamu wake)

  Jamaa huyo alikuwa amempeleka mkewe nyumbani ili kumjulisha kwa wazazi na wazee wa jamii yake.

  “Mapenzi yetu yalikuwa moto moto. Miezi mitatu baada ya kukutana tulianza kuishi kinyumba. Alitamani sana kukutana na wazazi wangu lakini sikuwa pazuri kifedha wakati huo kugharamia safari yetu,” alisema mfanyakazi huyo wa jua kali Ijumaa, Agosti 12, kulingana na Standard.

  Kila alipojaribu kujitetea ndivyo hasira zilimpanda babake na jamaa wa ukoo waliozidi kumpiga.

  “Isitoshe, baba sasa amenikana kama mtoto wake na kunifurusha kutoka kwa familia hiyo. Nilimfuata mke wangu Kibera kumueleza kwamba sikujua kile jamaa zangu walikuwa wakizungumzia,” akaongeza.

  Kisa hicho kinajiri siku chache tu baada ya jaji wa Mahakama Kuu ya Nairobi kusema kuwa uhusiano wa kimapenzi baina ya binamu sio haramu kisheria ingawa ni mwiko katika jamii nyingi Kenya.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku