• Breaking News

  Aug 17, 2016

  Mwenyekiti wa Kijiji Simanjiro Auawa Kwa Kupigwa Risasi

  Uhasama wa kisiasa katika kijiji cha kambi ya Chokaa wilaya ya Simanjiro umezidi kutisha uhai wa binadamu baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho Thomas Ratoi Molel kuuawa kwa kupigwa risasi ikiwa ni mtu wa pili anayedaiwa kuuawa kwa tofauti za kisiasa huku Msemaji Mkuu wa CCM Christopher Olesendeka akidai kuwa CCM haitaendelea kuvumilia matendo hayo lazima hatua kali zichukuliwe bila kujali kuwa wauaji watakuwa ni wanachama wa CCM au kutoka vyama vingine.

  Akiongoza misa ya maziko ya mwenyekiti huyo wa kijiji cha kambi ya chokaa thomas molel maarufu kwa jina la mbuki askofu mkuu mstaafu wa Kanisa KKKT Diosisi ya Kaskazini Dk Maritin Shayo amesema  kwa hali ilivyo  hivi sasa kuna haja ya watanzania kufanya maombi ya  kina kutafuta amani ya Tanzania na wanasiasa inawabidi kuwa makini.

  Ndugu wa marehemu Mbuki wakaeleza tukio lilivyo tokea na kudai kuwa sababu ya kifo chake ni uhasama wa kisiasa uliyo shamiri kwenye kijiji hicho kwa zaidi ya miaka miwili sasa huku Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula akisema wameshaanza kuchukua hatua ya kubaini wauaji.

  Baadaye Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC kutoka Simanjiro Christopher Ole Sendeka akasema ili ni tukio la pili katika kijiji hicho lakini lazima dawa ipatikane ili kumaliza uhasama huo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku