• Breaking News

  Aug 1, 2016

  Mwili wa mchungaji wakutwa umeharibika chumbani

  Mkazi wa Mtaa wa Makuburi Kibangu jijini Dar es Salaam, Frank Malusi amekutwa amekufa baada ya majirani kusikia harufu kutoka chumbani kwake.

  Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime amesema hakuwa na taarifa kuhusu tukio hilo na kuahidi kulifuatilia.

  Malusi ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Maombezi lililopo Makuburi, hakuonekana kwa siku nne mfululizo, lakini hofu zaidi ilizuka baada ya kusikia harufu ikitoka kwenye chumba chake.

  Mwenyekiti wa mtaa huo, Moshi Kaftani amesema jana kuwa alipewa taarifa na mwenye nyumba ambayo Malusi alikuwa amepanga, Peter Mrema kwamba hawajamuona kwa siku nne.

  Kaftani amesema aliamua kutoa taarifa polisi, ambao walifika na kuvunja mlango na kukuta mwili wa Malusi ukiwa umeanza kuharibika. Alisema polisi waliuchukua mwili huo kwa uchunguzi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku