Aug 7, 2016

Mwinyi Ndiye Alikuwa Rais Bora Tanzania...

Kwangu Mimi Rais bora wa muda wote ni mwinyi!

Hawa wengine wanazengua tu story nyingi majukwaani lakini wameshindwa kuboresha maisha ya wananchi!

Kwangu Mimi Rais bora ni Nani?
Rais bora ni yule anayeraisisha maisha ya watu wake yawe bora zaidi (sustainable life) katika kipindi chake cha utawala!!

Pamoja na mapungufu yake mengi lakini aliweza kuleta mabadiliko ambayo bila kuwa na hicho la tatu huwezi kuona alichokifanya!!!

Investment (uwekezaji) unapofanikiwa kwenye ili swala la uwekezaji hasa kwa kuwafanya wazawa kuwekeza bila vikwazo unapata credit kubwa kwa wananchi wako.

Mwinyi ndiye aliamasisha uwekezaji wa kiwango kikubwa hasa kwa wazalendo (wazawa) na mtakubaliana na Mimi kuwa hata matajiri wengi tulionao sasa wameupata utajiri wao katika kipindi cha mwinyi!!
Watu Kama

Reginald Mengi
Antony Dialo
Bakiresa

Baba yangu pia ananiambia ingawa nyerere aliwabana lakini mwinyi ndiye alimfanya apate pate pesa !!

Na wengine wengi wamepata pesa zao kipindi hiki bahati nzuri wamefanikiwa kuwekeza ndani ya nchi yao na kuajiri maelfu ya watanzania!!

Viwanda baadhi viliendelea kuwepo lakini vikaja kupoteza kipindi cha Mkapa

Pesa yetu ilikuwa imara dhidi ya dollar

Watu wengi waliobanwa na nyerere walitoa pesa zao na kuwekeza na kuongeza Ajira kipindi cha mwinyi!!

Nafikiri hata niwapongeze baadhi ya watu wenye asili ya Zanzibar kwa kutokuwa mafisadi!

Nimekuwa nikifatilia kashifa za ufisadi Tanzania toka kipindi cha mkapa sijawai kumsikia mzanzibar kakwapua !!

Sisikii kashifa za ufisadi katika selikari ya Zanzibar !!

Wabara inabidi tujimulike sana CUF pamoja na kuwa na ushawishi Zanzibar agenda yao kubwa sio ufisadi ni huduma kwa mwananchi na swala la muungano!!!

By Technically

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR