• Breaking News

  Aug 14, 2016

  Ni kweli Serikali imekataza vyombo vya habari kuripoti maandamano ya CHADEMA?

  Serikali ilipiga marufuku maandamano pamoja mikiutano isiyo rasmi lakini kuna taarifa zimekuwa zikisambaa kwamba Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye amepiga marufuku vyombo vya habari kuripoti taarifa za maandamano na vitakavyokiuka kuchukuliwa hatua.

  Waziri Nape Nnauye kwenye exclusive akititupa ufafanuzi ambaye anasema…
  ’Sijazuia vyombo vya habari kuripoti maandamano na mikutano lakini ukiripoti uchochezi na wewe unakuwa sehemu ya uchochezi‘

  ‘Lakini haiwezekani yanatolewa matusi ya nguoni alafu yakaripotiwa eti kwakuwa yamesemwa na mtu, chombo hicho hakitabaki salama‘

  ‘Kwamaana hiyo vyombo vya habari visishiriki kuripoti habari za uchochezi nilazima watumie akili ili wasiwe sehemu ya uvunjifu wa amani‘

  Ni adhabu gani zitatolewa kwa mwandishi ama chombo kitakachoripoti uchochezi? Waziri Nape kafunguka tena ‘Adhabu zitolewazo kwa vyombo vinavyoripoti uchochezi ni pamoja na kufutwa kabisa katika orodha ya vyombo vya habari‘

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku