Aug 14, 2016

Nigeria Yatinga Nusu Fainali Olimpiki

Timu ya taifa ya wanaume chini ya miaka 23 ya Nigeria imeichapa Denmark kwa mabao 2-0 na kutinga nusu fainali ya mashindano ya Olimpiki 2016 yanayoendelea jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Kwa mantiki hiyo, Nigeria chini ya nahodha wake John Obi Mikel itacheza na Ujerumani ambayo mapema iliichabanga Ureno 4-0.

Mechi hiyo itafanyika katika uwanja wa Fonte Nova huko Rio de Janeiro.

Mikel, kiungo wa Chelsea, aliwapa Nigeria bao la kwanza dakika ya 16 ya mchezo baada ya Imoh Ezekiel kupiga krosi maridadi.

Nigeria ingeweza kwenda mapumziko ikiwa na zaidi ya bao hilo mashuti ya washambuliaji wake hayakulenga lango.

Huku wakilisakama lango la Denmark, vijana hao wa Afrika walipata kona iliyochongwa na Mikel Obi katika dakika ya 59, ndipo Aminu Umar alipoiunganisha kimiani moja kwa moja akitumia kichwa.

Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com