Aug 5, 2016

Obama Ammwagia Sifa Mtanzania, Geline Fuko Kwenye Hotuba yake

Rais wa Marekani, Barack Obama amemwagia sifa Mtanzania Geline Fuko ambaye ni Mwanaharakati wa haki za binadamu, kwenye hotuba yake ya kwenye mkutano wa vijana Washington DC, Marekani.

Obama amekutana na vijana mbalimbali kutoka bara la Afrika ikiwa ni mpango wa serikali yake kila mwaka toka mwaka 2014 kukutana na vijana hao ambao wanaohusika na kuivusha jamii kwenye masuala mbalimbali ikiwemo biashara na siasa.

Geline Fuko

Rais Obama alimsifia Geline kutokana na juhudi zake za kuwawezesha watanzania kusoma katiba ya nchi kupitia simu za mkononi. Tazama video ya Obama akimsifia Mtanzania huyo.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR