• Breaking News

  Aug 12, 2016

  Olimpiki: Mfahamu Mwana Michezo Mdogo Kuliko Wote

  Macho, akili na masikio ya wapenda michezo wote duniani kwa sasa yapo nchini Brazil kwenye mashindano yanayoendelea ya Olimpiki.

  Mpaka sasa Marekani imefanikiwa kuongoza kutwaa medali nyingi ikiwa ni jumla ya medali 38 ambazo wamefanikiwa kuzipata wakifuatiwa na China (30), Japan (22), Australia (15) na nafasi ya tano imechukuliwa na Korea Kusini waliopata medali 11.

  Kitu kikubwa zaidi cha kufurahisha na kuvutia kwenye mashindano hayo ni kuwepo kwa muogeleaji mwenye umri mdogo kuliko wote kutoka nchini Nepal, Gaurika Singh (13).

  Gaurika ambaye anaiwakilisha nchi hiyo kwenye mashindano hayo amedai kuwa hapo awali hakuwa na uhakika kama atashiriki mwaka huu kutokana na kuwa mdogo kiumri na badala yake alifikiria kushiriki kwenye mashindano hayo mwaka 2020.

  Aidha binti huyo ameongeza kuwa hakuwa anaupenda mchezo huo hapo mwanzo lakini baba yake ndiye aliyemlazimisha kujifunza mchezo huo wa kuogelea na baadaye aliupenda baada ya kufundishwa.

  Gaurika ameanza kushiriki mashindano ya kuogelea tangu mwaka 2014 na tayari ameshashiriki kwenye mashindano kwenye nchi kadhaa ikiwemo Urusi, India, Ireland, Dubai na nchi nyingine nyingi.

  Kwa sasa Gaurika anaishi nchini Uingereza huku akiendelea kufundishwa mchezo huo na walimu wake wawili ambao ni Rhys Gormley na Christine Green.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku