Mwanariadha kutoka nchini Afrika Kusini, Caster Semenya amefanikiwa kuingia nusu fainali ya mbio za mita 800 kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea nchini Brazil.

Semanya (25) amefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kutumia muda wa 1:59.31 kumaliza hatua ya robo fainali ya mbio hizo lakini baadhi ya vyombo mbalimbali vimepinga ushindi wake huo kwa madai kuwa maumbile yake hayamhitaji kushiriki kwenye mashindano ya wanawake.

Hiyo siyo mara ya kwanza kwa Semanya kuingia kwenye utata huo. Hata mwaka 2009 alifanikiwa kushinda kwenye mashindano ya riadha yaliyofanyika huko Berlin lakini IAAF ilimtaka kupimwa juu ya maumbile yake lakini alifanikiwa kushinda kesi hiyo.


Post a Comment

 
Top