Aug 28, 2016

PAUL Makonda: Marufuku Viongozi wa Dini kupanga Foleni Ofisi za Wakuu wa Wilaya

Paul Makonda na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepiga marufuku viongozi wa dini kupanga foleni wanapokwenda katika ofisi za wakuu wa wilaya wa mkoa huo. 

Makonda ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Baraza kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) 

"Natoa wito kwa wakuu wa wilaya wote katika mkoa wangu, ni marufuku kumkuta kiongozi wa dini kupanga foleni katika ofisi zenu,hawa watu lazima waheshimiwe kama viongozi wengine wanavyoheshimiwa "alisema 

Kuhusu ujenzi wa ofisi za Bakwata, Makonda amesema kuwa ujenzi huo umefadhiliwa na mfuko wa GSM. 

" GSM foundation ndio inayojenga ofisi za Bakwata hivyo jamii inayonunua bidhaa za GSM ijue kuwa fedha wanazotoa zitarudi kwa jamii "alisema 

Mufti mkuu wa Tanzania sheikh Abubakar Zubairy bin Ally, amewataka waumini wa dini ya kiislaam kuachana na dhana potofu ya kuwa jengo hilo si halali kutokana na jitihada za ujenzi wake kufanywa na muumini wa kikristo. 

" Katu hatutashtushwa na kejeli za mitandaoni, Mkuu wa mkoa anayohaki ya kusaidia jamii ambayo imezungukwa na makundi mbalimbali ya dini "alisema.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR