Aug 6, 2016

Polisi wamsaka Dk Mwaka


Kamishina msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdan amesema bado wanamtafuta mmiliki wa kampuni ya Foreplan Juma Mwaka kama walivyoagizwa na Naibu Waziri wa Afya.

Alisema vijana wake wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24 kama walivyoagizwa hapo jana.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk  Hamisi Kigwangalla la kumtafuta baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo na kukuta huduma zinaendelea.

Akiwa katika jengo hilo akikagua ndani mara baada ya kupata kibali cha Polisi cha kufanya upekuzi, wateja wa Dk Mwaka walikuwa wanaendelea kuingia kufuata huduma ya matibabu huku wengi wao wakiwa kina mama.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR