Aug 20, 2016

Rais Obama Achukizwa na Tabia ya Mwanae Malia Baada ya Kunaswa Akipuliza Bangi

Kama inavyotegemewa kwa baba yeyote duniani, tabia ya binti yake, Malia imemkasirisha vibaya Rais wa Marekani, Barack Obama.

Hivi karibuni, Malia alionekana akivuta bangi kwenye tamasha moja maarufu.

Kwa mujibu wa tovuti ya RadarOnline, vitendo vya hivi karibuni vya Malia vimemsononesha sana Obama anayemaliza muda wake mwaka huu kama rais wa Marekani.

Awali, video ilisambaa mtandaoni ikimuonesha Malia Obama, 18, akionekana kuvuta bangi kwenye tamasha la Lollapalooza huko Chicago mwezi uliopita.

Kisha Malia alihudhuria kwenye party iliyopo kwenye kisiwa ambacho familia yake ipo mapumzikoni iliyofungwa na polisi. Malia alihitimu mwaka huu kwenye shule maalum ya Sidwell Friends ya Washington, DC, na anatarajiwa kujiunga na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2017.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR