• Breaking News

  Aug 25, 2016

  Rais, Unda Tume ya Kijaji Kuchunguza Mauaji ya Polisi, Pia Polisi ichunguzwe

  Magufuli
  Natoa pole kwa jeshi la polisi, Ndugu na jamaa za walifiwa katika tukio la mauaji ya Polisi wa nne pale CRDB Mbande...

  Nimefuatilia taarifa na maoni ya watanzania wengi tangu kutokea kwa tukio hili, kwakweli hiki ninachokiona ni hatari kwa usalama wa Taifa letu.

  Chuki hii ni kubwa, inahitaji suluhu ya haraka sana kunusuru taifa letu..... Ni hatari kuona mtu anayelindwa na askari usiku na mchana, kufurahia askari wake anapouawa na maadui.....

  Nitumie fursa hii, naamini Rais anaweza kusoma hapa ama yeyote yule anayepata fursa ya kusoma hapa atafikisha ujumbe huu,

  Mh Rais Magufuli, unda tume ya kijaji kuchunguza vifo vya askari wetu, pia kuchunguza uhasama uliopo kati ya raia na polisi , Kuna ukakasi kwenye taarifa za awali za mauaji haya. Jeshi la Polisi lisishiriki katika tume hiyo bali lichunguzwe nalo, pia vyama vya siasa kikiwemo chama tawala kichunguzwe.

  Lolote kwa sasa linawezekana... Kwani lisilowezekana mbinguni, hapa Tanzania linawezekana.

  NB

  Kama dhamira yako Mh ya kufanya mabadiliko ya kweli bado ipo, Muundo vya vyombo vya ulinzi na usalama ubadilishwe sasa... Muundo huu wa sasa ndio kikwazo kwa Tanzania kupata maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Huu ni mfumo wa karne ya 20 enzi za ukombozi wa bara la Afrika, sio hiii leo karne ya 21 tunapopambana kiuchumi hasa uchumi wa viwanda".

  By Yericko Nyerere

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku