• Breaking News

  Aug 5, 2016

  RC Makonda Ajihami..Akutana na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia. Ukonga jijini Dar leo

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Agosti 5, 2016 amekutana na Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam na kuzungumza nao maswala mbalimbali ya kiusalama kwa Mkoa wa Dar es salaam, huku akiwapongeza Askari hao kwa uzalendo wao kwa Taifa.

  "Hakuna wafanyakazi wazalendo nchini kama Askari, kwani wako tayari kufa ili taifa la Tanzania liwe salama, Pia uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu" alisema Makonda.

  Makonda amewaahidi Askari hao kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba waimarishe usalama wa Jiji la Dar es salaam, ili iwe kama Dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta, kwani Jiji hili linapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa.

  Makonda amewahakikishia askari hao kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt. John Magufuli, ombi la Makonda lilikua ni juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa ni pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika kwenye eneo la tukio bila kuchelewa.


   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katika Mkutano wake huo na Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam.


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza jambo na baadhi ya Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ukonga Jijini Dar es salaam.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku