• Breaking News

  Aug 8, 2016

  Sakata la Wizi wa Punda Simanjiro lachukua Sura Mpya..Punda Hamsini Wachunwa Ngozi


  Sakata la wizi wa wanyama aina ya Punda kihongo katika wilaya ya Simanjiro limechukua sura mpya baada ya watu wasiyo julikana kuiba  zaidi ya punda hamsini kwenye kijiji cha Naberera kisha kuwaua kuchuna ngozi na kuwatelekeza porini hali inayohashiria kushamiri kwa wizi wa wanyama hao tegemeo pekee kwa usafirishaji wa  mizogo kwa watu wa jamii ya kifugaji.

  ITV ilifika kwenye kijiji cha Naberera na kushuhudia mizoga ya Punda iliyochunwa ngozi na jutelekezwa porini ambapo wakazi wa eneo  hilo wamesema matukio hayo yawafanya kuendelea kuwa masikini kwakuwa Punda ndiyo mnyama pekee anayetegemewa kwa kusafirisha wagonjwa maji na bidhaa nyingine kwakuwa hakana magari.

  Baadhi ya wenyeviti wa vitongoji vilivyopatwa na mkasa huo wamesema hadi sasa ni zadi ya Punda mia sita wameshaibwa na hali hiyo isipo komeshwa itaweza kuleta mashadha  kwani wananchi wameanza kuwasaka wezi hao kwa silaha za jadi.

  Mwenyekiti wa kijiji cha Naberera Jacob Korosi amesema taarifa za wizi huo zimeshafisha kwenye ngazi mbalimbali bila mafaniko na kwamba kuna baadhi ya watendaji wanahusika kufanikisha wizi huo

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku