• Breaking News

  Aug 30, 2016

  Septemba 1, 2016 Makonda Asema JWTZ Watafanya Majaribio Mbalimbali ikiwemo Kurusha Ndege Angani

  Paul Makonda
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuunga mkono Jeshi la Wananchi litakalokuwa likitimiza miaka 52 tangu kuanzishwa kwake, Septemba Mosi, ambapo katika kusherehekea litafanya majaribio mbalimbali ikiwemo kurusha ndege angani.

  Makonda amewataka wakazi wa Jiji hilo kutokuwa na hofu pindi watakapoona majaribio hayo yatakayofanywa na Jeshi hilo.

  Amesema mbali na kufanya majaribio mbalimbali, Jeshi hilo pia litashiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.

  Akizungumzia ‘operesheni’ UKUTA, ambayo nayo imepangwa kufanyika Septemba Mosi, RC Makonda amedai kuwa UKUTA ni hatua ya mwisho ya mtu kufikiri na kwamba wao hawana kitu kinachoitwa UKUTA huku akitoa onyo kali kwa wale wote watakaoshiriki.

  “Watu wote wanaojua umuhimu wa amani ya nchi basi watatambua thamani ya maadhimisho ya Jeshi letu la Wananchi kwani leo hii tunakaa kwa amani kwasababu ya nguvu kubwa wanayoitumia katika kuilinda amani hiyo,” amesema RC Makonda.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku