Bombadier Q400
Serikali imesema iliamua kununua ndege mbili za abiria za aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo mjini.

Yamesemwa hayo Jumanne hii jijini Dar es Salaam na waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Ngarawa, wakati wa ufunguzi mafunzo ya wakufunzi wa Marubani katika chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT).

“Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi aina ya ndege za kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahususi ya kuhudumia usafiri wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia shirika la ndege Tanzania (ATCL)”,alisema Profesa Ngarawa.

Ndege hizo zinatarajiwa kuanza safari za ndani hivi karibuni.


Post a Comment

 
Top