Aug 19, 2016

Siasa za Kihuni Hazitajenga Tanzania

Bunge
Hata siku moja hatutafanikiwa kuijenga nchi yetu iwe imara kiuchumi na kijamii kwa kutegemea siasa za kihuni. Siasa ndiyo kila kitu kwenye maisha ya binadamu ingawa si kila binadamu anakuwa kwenye mfumo wa kisiasa!

Waliomo kwenye mfumo wa siasa (wanasiasa) ndiyo hasa wanaopanga mambo ya maendeleo kwa niaba ya wananchi wenzao ambao hawamo kwenye mfumo wa siasa. Lakini hapa Tanzania kumeibuka siasa za kihuni kwa baadhi ya wanasiasa kujifanya wao si wanasiasa bali wapinzani wao ndiyo wanasiasa.

Wakati mwingine utasikia "Hapa hatutaki siasa" au "siasa hazituletei chakula, elimu, matibabu au barabara" Lakini labda anayesema hivyo ni Rais, Waziri, Mkuu wa Mkoa au Wilaya, Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani na hata Mwenyekiti wa Mtaa, lakini hawa wasiotaka siasa si ndiyo wanasiasa wenyewe?

Yaani mwanasiasa anaposema hataki siasa si unakuwa uhuni? Ni kama vile Golikipa anamwambia fowadi wa timu pinzani hapa hatutaki kufungana kwani kufungana hakuleti furaha, hakuleti mvua wala siyo pumzi, lakini kwa nini Golikipa yupo uwanjani kama kufungana hakuleti yote hayo?

Jee mtu akichaguliwa kwenye nafasi hizo nilizotaja hapo juu za utumishi wa umma anakoma kuwa mwanasiasa? Kama anakoma kuwa mwanasiasa basi ni kwa nini Katiba ya nchi yetu inatambua kuwa chama cha siasa kikimnyang'anya Mbunge, Diwani, au Mwenyekiti wa Mtaa kadi ya chama husika mtu huyo anakoma kuwa kiongozi wa ngazi husika. Inakuwaje wasio wanasiasa utumishi wao ukomeshwe na chama cha siasa?

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR