Aug 15, 2016

Siku za Yaya Toure ndani ya Manchester City zahesabika

Katika kile kinachoonekana sasa hana nafasi kabisa ya kuendelea kuitumikia Manchester City, kiungo mkongwe Yaya Toure ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Steaua Bucharest, kesho Jumanne katika mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Toure ambaye ana umri wa miaka 33, hayumo katika mipango ya kocha wake mpya Pep Guardiola na hilo limeonekana kuanzia katika mechi ya kwanza ya msimu huu dhidi ya Sunderland ambapo hakujumuishwa katika kikosi cha kwanza.

Man City ipo Romania kwa ajili ya mchezo huo lakini kiungo huyo raia wa Ivory Coast hayumo hata katika orodha ya wachezaji 18 waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo.

Awali akizungumzia juu ya majaaliwa ya mteja wake, wakala wa Toure, Dimitri Seluk alisema ana imani kuwa Guardiola atampa nafasi Toure kuthibitisha ubora wake.

Mbali na Toure wachezaji wengine mastaa ambao hawajasafiri na timu hiyo ni Eliaquim Mangala, Samir Nasri na Wilfried Bony.

Toure yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake ambapo anaendelea kulipwa mshahara unaokadiriwa kuwa ni pauni 250,000 kwa wiki na inaonyesha kuwa hana maisha marefu klabuni hapo.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR