• Breaking News

  Aug 19, 2016

  Simba Hawawezi Kumdai Kessy, Watakiwa Kumlipa Mshahara Wake - Tippo

  MENEJA wa mchezaji Hassan Ramadhan ‘Kessy’ amesema kuwa Simba hawawezi kumdai mchezaji wake huyo au klabu ya Yanga kwani bado anawadai mshahara wa miezi 3 kuanzia April 2016.

  Akizungumza na GLOBU YA JAMII, Tippo  Athuman ameeleza kuwa Simba wanatakiwa kumlipa Kessy mshahara wake na kulingana na kanuni na sheria za mkataba kama klabu itashindwa kumlipa mchezaji mshahara wake basi ana uwezo wa kuvunja mkataba nao.

  Tippo amesema, Kessy atacheza kwenye klabu yake ya Yanga aliyosajiliwa, na Simba wasitake kutumia fursa hiyo kujipatia hela wakati wanajua walishavunja makubaliano ya mkataba. “Simba wanataka kujipatia hela kupitia Kessy wakati wanajua kuwa walishakiuka mkataba kwani hawajamlipa mshahara wa miezi mitatu kuanzia April mwaka huu”.

  Kufuatia sakata la mchezaji huyo kusikika kila wakati katika vyombo vya habari, Kamati ya Sheria na Haki za wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wote wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku  jina la Hassan Ramadhani ‘Kesi’ likipitishwa kuitumikia Young Africans kuanzia msimu huu 2016/17.

  Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa imepitia usajili wa timu zote na kujiridhisha kwamba suala la mchezaji Hassan Kessy limeegemea kwenye madai na si usajili ambako Simba ndiye mdai kwa kumtuhumu mchezaji huyo kuwa alianza kuitumikia Young Africans kabla ya kumaliza mkataba wake Simba SC. Mkataba wake ulifika mwisho, Juni 15, 2016.

  Kama ni madai Simba inaweza kuendelea kumdai Kessy au Young Africans wakati mchezaji huyo anatumika uwanjani kwa mwajiri mpya. TFF inafuatilia na kuangalia haki ya Simba namna ya kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa zamani.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku