Machinga Akikamatwa na Wanamgambo
Waziri Simbachawene amesikika asubuhi hii akifafanua kuwa amri ya Rais Magufuli aliyoitoa huko kanda ya ziwa kuhusu machinga kuruhusiwa kufanya biashara bila vizingiti ilikuwa inalihusu eneo alilolikusudia na siyo hadi Dar es Salaam au kwingineko.

Ameongeza kwa kumuamuru RC Makonda kuhakikisha machinga wanarudi kule Mchikichini na maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili yao.

Chanzo: Radio One (kipindi cha Nipashe asubuhi leo 27 August 2016).

My Take: Kuna umuhimu wa kuongeza kwenye job description ya mawaziri kipengele kinachosema "Kufafanua matamko ya rais".


Post a Comment

 
Top