• Breaking News

  Aug 8, 2016

  Taarifa ya Oscar Pistorius Kudaiwa Kujaribu Kujiua Akiwa Gerezani

  Oscar Pistoriuos mwanariadha wa South Africa ambae alimiliki vichwa vya habari baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp.

  August 6 2016 iliripotiwa taarifa za Pistorius kukimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha kwenye mikono, taarifa zilizopatikana kwa wafungwa wenzake ni kwamba alifanya hivyo kwa makusudi.

  Taarifa iliyoripotiwa hivi punde ni kwamba Pistorius amerejeshwa gerezani baada ya kupata matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyoyapata. Msemaji wa gereza alisema majeraha hayo yalikuwa ‘madogo’ na kwamba amerudishwa gerezani.

  Aidha msemaji wa gereza ameongeza kuwa Pistorius amekanusha taarifa zilizotolewa kuwa amefanya hivyo kwa kukusudia na kuwa alitaka kujiua.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku