• Breaking News

  Aug 17, 2016

  Tanzania ya Kwanza Kati ya Nchi zitakazotembelewa na Watalii Mwaka Huu

  Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kati ya orodha ya nchi kumi bora duniani zitakazotembelewa na watalii mwaka huu.

  Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mtandao wa kimataifa wa usafiri wa anasa wa Marekani Virtuoso, Tanzania imepata asilimia 98, ikifuatiwa na Ureno asilimia 88 na Ireland 58.

  Nchi nyingine na asilimia kwenye mabano ni Brazil (53), Mexico (48), Urusi (44), Uholanzi  (38), Jamaica (28).Nchi nyingine ni Sweden (28) na Poland (18).

  “Tanzania inajivunia ongezeko kubwa la watalii  watalii wanaotarajia kusafiri katika msimu huu ili kuja nchini kufuata maajabu mbalimbali ikiwemo, ” taarifa za mtandao huo zimesema.

  Akizungumzia hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga alisema  hayo ni mafanikio makubwa kwa Tanzania katika sekta ya utalii.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku