Tanzania imeshika nafasi ya 58 kati ya nchi 67 duniani katika orodha ya maeneo yanayopendwa zaidi na wataalamu duniani barani Afrika.

Orodha hiyo imetolewa leo na Utafiti wa Kimataifa wa Expat Insider ulioangalia nchi inayopendwa zaidi na wataalamu wa nje ya nchi hiyo wakiangalia vigezo vya eneo lililo rahisi kuishi, kujifunga lugha inayotumiwa na wakaazi na maisha bora ya kifamilia.

Katika utafiti huo, Uganda imeongoza katika bara la Afrika kwa kushika nafasi ya 25 duniani huku Kenya ikishika nafasi ya 46 na ni ya pili barani Afrika.

Ingawa Tanzania imeshika nafasi hiyo lakini Nigeria imekuwa ya mwisho katika utafiti huo kutokana na hali ya gharama ya kuishi lakini limeonekana kuimarika ukilinganisha na mwaka uliopita.

Chanzo: Mwananchi


Post a Comment

 
Top