Aug 17, 2016

TCRA Waja na Kampeni Hii Kudhibiti Makosa ya Mtandaoni

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) James Kilaba amewataka wadau wa mawasiliano nchini kujiepusha na sheria za ukiukwaji wa mitandao kwa kutokusambaza ujumbe ulio na maudhui ya uchochezi na uzushi.

James Kilaba ameyasema hayo wakati akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam  juu ya matumizi sahihi na salama ya mitandao mbapo amesema kuwa watumiaji wa mitandao wanatakiwa kutotoa maudhui ya uchochezi pindi wanapo pokea ujumbe huo kwa mtu mwingine.

“Nina wataka mfute maramoja pindi mnapopokea taarifa za uchochezi na kutoa taarifa kwa wanaohusika mnazipokea taarifa hizo” Alisema Kilaba.

Kilaba ameongeza kuwa watuamiaji wa mitandao wasitengeneze akaunti kwa lengo la kufanya utapeli au kutumia taarifa zisizo za kwao na kusisitiza kuwa wanatakiwa kutunza vifaa wanavyohifadhia kumbukumbu zao.

Kufuatia hali hiyo TCRA wamezindua kampeni ya TZ-CERT(Tanzania Computer Emergency Response Team) kwa lengo la kuongeza ufahamu kwa watumiaji wote wa mtandao baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto kwa watumiaji wa mitandao, hivyo kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi mitatu kupitia mtandao wa Facebook, Twitter.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR