• Breaking News

  Aug 5, 2016

  TFF yamuita Jerry Muro Kimtindo...


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeibuka kwa kusema kuwa ruksa kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mwasiliano wa Yanga, Jerry Muro kukata rufaa iwapo anahisi hakutendewa haki.

  Muro amefungiwa na TFF hivi karibuni kufuatia madai ya kulishambulia shirikisho hilo ambapo atalazimika kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja.

  Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa TFF, Afred Lucas amefunguka kuwa, kuna taarifa wamezipata kuwa Muro yupo mbioni kukata rufaa na kudai kuwa kwa upande wa shirikisho hilo halina tatizo linasubiri rufaa hiyo na watasimamia haki.

  Aidha, alieleza kuwa, madai ya kwamba bado hajapata barua ya kusimamishwa si ya kweli na kudai barua ambayo haijamfikia ni ya hukumu ya kesi yake.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku