• Breaking News

  Aug 16, 2016

  UCHAMBUZI: Mkuu wa Mkoa Anapata Wapi Tshs. Bilioni Nne za Kutoa Msaada? Anatumika?

  Mkuu wa mkoa yeyote yule katika mikoa ya Tanzania hana chanzo chochote kile cha mapato kinachomuwezesha kuwa mtu wa kutoa misaada kwenye jamii hasa hasa fedha nyingi ambazo hata akikusanya vipi mishahara yake yote hawezi kufanya hivyo. Mkuu wa mkoa ni mtumishi tu ambaye kazi yake ni kusimamia shughuli zote za kijamii na ulinzi ndani ya mkoa wake, pia kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM.

  Mkuu wa mkoa hana mamlaka yoyote ile ya kukusanya mapato ndani ya mkoa wake, hana mfuko wa fedha kutoka serikali kuu. Yeye ni msimamizi tu wa kuhakikisha kuwa mapato yote na fedha zote zinatumika kama ilivyopangwa na mabaraza ya serikali za mitaa ndani ya mkoa wake.

  Sasa ni ajabu sana tena sana kusikia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiahidi msaada wa Tshs. bilioni nne eti kujenga ofisi ya kisasa ya taasisi ya kidini (BAKWATA)! Kwa fedha zipi? Zilipatikana kwa njia gani?

  Sasa basi, je Paul Makonda anatumika? Upo uwezekano mkubwa sana kuwa huenda kauli ya Paul Makonda ina mkono mzito tena wenye dola nyuma yake na ndiyo maana amekiuka waziwazi misingi yake ya uwajibikaji tena kwa kujiamini (with impunity)

  Sasa swali ambalo wana Jamii forum tunalotakiwa kujiuliza tena sana na kujadili kwa mapana ni; Je ni nini hasa nia ya jambo hili na hatima yake siku za usoni? Lina madhara gani ya kijamii mbeleni? Ni kwanini iwe kwa Paul Makonda mtu ambaye kujihusisha kwake na jambo hili kunaleta taswira hasi kabisa mbele ya uso wake kijamii?

  Imeandikwa na G Sam/ Jamii Forums

  1 comment:

  1. Si Kweli. Kwa nini ni yeye pekee. Na hata kama amechangiwa hii ni mali ya umma inabidi serikali ipokee na iamue vipi itatumika. Na kama alifanya harambee ataje ni nani kaoa na je anarisiti? ni kama NGO anapopewa pesa inabidi azidiclare wapi kapata iwe wazi. Nyinyi mnaotetea ndio hamzijui sheria. Kuna tofauti gani hii na rushwa? CCM jiangalieni jamani kama chama kimeendeshwa namna hii kwa muda wote ni rahisi kuiba. labda kapewa billioni nne nyingine mfukoni. Ebu fuatilieni hili jambo kwa ukaribu na muwajibu Watanzania na msifunike mambo.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku