• Breaking News

  Aug 10, 2016

  UDART imezindua Mpango wa Kuongezea Malipo ya Nauli Katika Kadi

  Kampuni ya kusafirisha abiria jijini DAR ES SALAAM,UDART imezindua mpango wa kuongezea malipo ya nauli katika kadi zenye kiwango cha fedha kinachomuwezesha abiria kutumia huduma ya mabasi ya kwenda haraka,mahala popote ambapo wakala wao walieingia nae mkataba yupo.

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini,msemaji wa kampuni ya UDART DEUS BUGAYWA,amesema kwa muda mrefu tangu walipozindua huduma ya mabasi hayo,wasafiri waliokuwa wanatumia kadi hizo hawakuwa na eneo jengine la kuongeza fedha katika kadi kwa ajili ya kulipia nauli bali iliwalazimu kufika vituo vya UDART ili kuongeza fedha.

  Amesema kwa sasa huduma hiyo ya kuongeza fedha imekabidhiwa kwa mawakala wao waliopo maeneo mbali na vituo vyao ili kuwarahishia uongezaji wa fedha kwenye kadi zao mahala popote.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku