• Breaking News

  Aug 27, 2016

  Uhuni Wanaofanya Traffic Kwa kutumia Mashine EFD. Serikali iangalie hili

  Kutokana na Huu utaratibu mzuri lakini pia wenye changamoto wa kulipia makosa kupitia mashine za EFD na wakat mwingine kukopeshwa ikiwa hulipi cash. Askari wetu wameanza kufanya uhuni. Wanalazimisha makosa ambayo hayapo au hayakupaswa kuwa ya adhabu kutokana na maelezo mtuhumiwa anayotoa.

  Juzi nlitoka kazini kurudi nyumban na bahati mbaya au nzuri nikasimamishwa na Traffic. Akakagua kila kitu akakuta kipo sawa. Akataka niwashe taa na kuzima kama mara 3 hivi akaona haitoshi akamwita mwenzie aje asimame mbele halafu yeye ndo awashe taa.mara ikaonekana katika head lamps kuna taa haiwak.

  Haraka akanambia taa yangu haiweki nlishangaa maana ilikuwa inawaka kweli nlipowasha ikawa haiwek hivyo mwanga taa moja kubwa umepungua. Lakini nilimweleza kuwa taa zote zilikuwa zinawaka.lakini pia yale ni mambo ya umeme muda wowote inaweza tokea tatizo.yule mzee alikataa kabisa akisisitiza nimalizane naye...muda umeenda naye anataka akamilishe mahesabu.nlimlipe chake aondoke.akasisitiza sana.nami sikuwa naona kuna haja ya kumpa pesa. Basi nikamwambia sina haraka akaenda mbele ya gari kwa hasira akaandika namba zake kwenye ile mashine na kurud kwangu.

  Akanambia "hujanikomoa kitu hata hii unayolipa kwa mkopo kuna tsh 5000 yangu inatoka humu ndani inakuja kwangu. Sasa sijui umekwepa nini.ungenipa ya kung'arishia kiatu usingekaa hapa kupoteza muda"

  Kauli hii ilinikwaza sana ni vile tu nimekuwa mstaarabu lakini niliwaza mambo mengi mabaya mabaya kichwan. Nikakumbuka kwa nini kuna watu huwagonga traffic.pengine ni sababu kma hizi.anyway.mi nmemsamehe.

  Lakini je ni kweli kuwa traffic wanaopewa mashine wanapewa na kiwango cha pesa za kukusanya kwa siku?na je kuepuka raia wasinyanyaswe au kulazimishwa rushwa nini kifanyike?

  Nashauri kuwe na karatasi ya kusign kuonesha kuwa raia karidhishwa na adhabu kuepuka uhuni unaofanyika na traffic kwa sasa.serikali kusanyeni mapato.ila msiwatese raia hawa maskini kwa mzigo ambao ni wa uonevu kwa vile tu ninyi wakubwa tunawanunulia mafuta ya gari zenu na kuwafanyia service. Je hakuna adhabu za kutoa onyo tu?

  1 comment:

  1. vSiku njema Mimi ni binafsi Taasisi mkopo, i unataka kuwajulisha wote kwamba sisi kutoa kila aina ya mkopo kama vile mkopo madeni ya kuimarishwa mkopo ofisi mkopo wa biashara binafsi mkopo
   mkopo nyumba refinancing mkopo na hivyo zaidi katika chini
   riba ya 3%. Kama nia ya kuwasiliana nasi kwa siku.
   kupitia barua pepe: edmark.co.Ltd@gmail.com

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku